Mastaa wengi wamekuwa
hawadumu kwenye ndoa zao na wengine kwenye uhusiano wao wa kimapenzi.
Ukijaribu kumuuliza kijana yeyote mwenye nia ya kuoa atakuambia bora aoe
mwanamke wa kawaida kuliko staa.
Si suala la kuoa tu,
hata kwenye mapenzi ya kawaida ni wachache wanaoanzisha uhusiano na
mastaa wakiwa na ndoto za kudumu kwa muda mrefu. Ukiona kijana
‘anamsalandia’ staa ujue ni ili amuonje tu kisha amtose.
Pia ukifuatilia
utagundua kuwa, mwanamke wa kawaida akitokea kumpenda staa wa kiume,
anatafuta ile sifa ya kuwa naye lakini anajua hawezi kudumu
naye.Kutokana na hilo sasa, makala haya yanajaribu kukupa kwa ufupi
sababu 10 ambazo zinawafanya mastaa wengi wa kike kutodumu kwenye ndoa.
Tamaa
Hili lipo sana kwa
mastaa wa kike. Baadhi yao wana tamaa ya kuwa na maisha f’lani ili
waonekane nao wamo wakati uwezo haupo. Matokeo yake sasa akiolewa na
mwanaume ambaye hana kitu, akimpata wa pembeni ‘pedeshee’ wa kumtunza,
kwa tamaa zao hujikuta wakisaliti.
Unakuta msichana kwa
kuwa ni staa, anataka awe na gari zuri, abadili nguo kila siku, simu
kali na vitu vingine vya thamani wakati pesa hana na mume naye ni
kapuku. Hapo ndipo wengi huamua kuchepuka na matokeo yake sasa hajali
tena ndoa.
Ustaa mwingi
Mastaa wengi
wakishajitambua kuwa wao maarufu, basi hata kwa wapenzi wao wanaleta
zile nyodo za ustaa. Wanasahau kuwa hata rais anapokuwa na mkewe
humnyenyekea kama mke na mambo mengine kuendelea.
Utakuta staa anataka kuonesha ustaa wake kwa mumewe, yaani anataka mume awe chini yeye awe juu kisa tu anatikisa jiji.
Halima Yahaya ‘Davina.
Unyenyekevu katika
mapenzi unakuwa haupo, eti anajipa imani kwamba hata akiachwa kwa kuwa
anapapatikiwa na wanaume wengine kutokana na ustaa wake, hatakosa wa
kumchukua. Hiyo ni dhana potofu!
Uvivu, kupenda kulala…
Baadhi ya mastaa hata
wakiolewa wanashindwa kuvaa joho la ‘mke wa mtu’. Wanapenda kukaa tu na
kuletewa kila kitu nyumbani. Akicheza muvi moja na kujulikana basi
anaona dunia ndiyo yake, hakumbuki kutafuta kazi ya uhakika.
Usiku atapenda atoke, mchana ni mtu wa kulala tu kisa kachoka. Ni mwanaume wa aina gani atakayemvumilia?
Starehe kwa sana
Mke wa mtu hata kama
anastahili kustarehe siku mojamoja, lakini baadhi ya mastaa walioingia
kwenye ndoa huona wao starehe lazima ichukue sehemu kubwa ya maisha yao.
Atalazimisha kila siku watoke na hata kama mume atakuwa si mtu wa
kuendekeza mambo hayo, yeye ataomba awe anaenda na mastaa wenzake,
akikataliwa inakuwa tatizo.
Hawajitambui
Mastaa wengi wanakosa
elimu ya kujitambua. Ndiyo maana wengi wanaitwa malimbukeni. Unakuta
staa amepata mume mzuri tu lakini yeye anashindwa kujitambua kuwa yeye
ni mke wa mtu asiyestahili kuingiza ustaa wake kwenye maisha yake ya
nyumbani.
Ndoa fasheni
Jaribu kuchunguza
utagundua kuwa, mastaa wengi wanaolewa kama fasheni. Utamkuta staa wa
kike anasema wazi kwamba, amechangia wengi sana hivyo na yeye anataka
kuchangiwa hivyo analazimisha kuolewa.
Wanaoolewa kwa sababu
hiyo ni wale ambao hata ndoa zao zikivunjika hawaoni hatari, wanaona ni
sawa tu kwa sababu angalau wameonja ndoa!
Judith Wambura ‘Jide’.
Uvumilivu wa shida
Mara nyingi watu wanapooana hukubaliana kuishi pamoja kwa shida na raha. Mastaa wengi hawataki shida, wao wanataka raha tu.
Matokeo yake sasa ukiona
mambo yanaenda kombo, ni wachache sana wanaoweza kuvumilia shida. Wengi
wataanza visa na hatimaye wataomba talaka au kuamua kutoka kwenye ndoa!
Dhana potofu
dhidi yao
Mastaa wengi wanaonekana
si watu wa kuolewa. Sasa anapotokea mwanaume wa kumuoa staa, hata
kwenye mambo ya kawaida ataona anafanyiwa hivyo kwa sababu ya
ustaa.Matokeo yake sasa, hata kama staa huyo atajitahidi ili adumu
kwenye ndoa yake atashangaa ile damu ya ustaa inamtesa.
Wanakosa staha
Mke kama mke lazima awe
na staha, kitu ambacho baadhi ya mastaa wanakikosa. Utakuta staa kaolewa
lakini ana marafiki wengi wa kiume na anataka mume wake asihoji juu ya
urafiki wao.Kama ni msanii akiwa lokesheni, afanyiwe lolote na wanaume,
avae nguo hata za utupu kisa eti anaigiza. Mbaya zaidi si lokesheni,
hata nje ya fani wanataka kuishi kisanii.
Jack Patrick.
Wako tayari kuachika
Mastaa wengi wa kike
wakiolewa, wanakaa mkao wa kuachika wakati wowote. Ni wachache
wanaofanya jitihada za kutunza ndoa zao. Yaani wanatembea kwenye ile
dhana potofu kwamba staa hawezi kudumu kwenye ndoa.
Sababu hizo hapo juu na
nyinginezo ndizo zilizosababisha ndoa za mastaa kama vile Nuru Nasoro
‘Nora’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jack Patrick, Aunt Ezekiel’, Salome
Urasa ‘Thea’, Halima Yahaya ‘Davina’, Judith Wambura ‘Jide’, Stara
Thomas na wengineo kuvunjika.
0 comments:
Post a Comment