MTANDAO
wa wanafunzi Tanzania (TSNP) umeipa siku saba Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kutoa ufumbuzi juu ya namna gani wanafunzi wenye sifa za kupiga
kura watakavyoandikishwa kwenye mfumo mpya wa Biometric Voters
Registration (BVR) kufuatia kuingiliana na ratiba za masomo.
Tamko
hilo limetolewa jana Jijini Dar es salaam, kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti
wa umoja huo Shitindi Venance, ambapo alisema kuwa wanaiomba tume hiyo
ya uchaguzi ndani ya siku saba kueleza ni kwa namna gani wanafunzi
waliko vyuoni pamoja na wale waliko bonding wenye sifa za kupiga kura
namna watakavyoandikishwa kutokana na ratiba za uandikishaji kupishana
na zile za vyuo pamoja na shule za Sekondali.
Alisema
kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa kwa upande wa wanafunzi nchini
zinazopelekea mtandao huo kuwa na sintofahamu juu ya hatma ya
undikishwaji wa wanafunzi wenye sifa za kuandikishwa kwa mujibu wa
katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Nec.
“Mtandao
huu umekuwa ukifuatilia kwa ukaribu sana mchakato wa uandikishwaji
tangua kuanza kwake kupitia matawi yake yaliyoko mikoani matharani
Njombe, Ruvuma, Mtwara na Mbeya na kubaini kuwa kundi la wanafunzi
limekuwa na changamoto kubwa kwenye zoezi la uandikishwaji,
“Hii
ni kutokana na ukweli kwamba zoezi la uandikishwaji linaendelea wakati
huo huo wanafunzi wakiendelea na ratiba zao za masomo huku wengine
wakiwa shule za bweni,
“Hivyo
kama tume tunasikitika kwani tume ya uchaguzi inayatambua haya lakini
bado haitaki kutoa mwongozo ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye sifa
wanapata haki yao ya kuandikishwa, hivyo tunatoa siku saba kuanzia kesho
(leo) tume itupe majibu, ” alisema Venance.
Aliongeza
kuwa ni bora NEC ikapeleka mashine (BVR)kwenye kila taasisi ya elimu
kwaajili ya uandikishwaji wa wanafunzi wakiwa katika taasisi zao kama
walivyofanya NIDA.
Lakini
pia wanaiomba tume kuhakikisha kuwa inatoa majibu juu ya changamoto
hiyo inayowakabili wanafunzi katika kwenye zoezi hilo kwani ni hatari
kwa Amani ya Nchi endapo wanafunzi na wanavyuo watakosa haki yao ya
kuandikishwa na hatimaye kukosa haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi
ujao.
Kwa
upande mwingine umoja huo umeitaka serikali kuanza kushughulikia vyanzo
vya mogogoro na siyo matokeo ya migogoro hivyo watawala wa vyuo vikuu
nchini watumie busara ya kuwarudisha wanafunzi wote waliofukuzwa na
wengine kusimamishwa kwani ni hatari kwa amani ya nchi .
0 comments:
Post a Comment