Mazoezi ni miongoni mwa vitu, vinavyosisitizwa na wataalamu wa afya kwa ustawi wa mwili wa binadamu huku yakiwa na mchango mkubwa katika kuukinga mwili na marathi mbalimbali.
Mwili wa binadamu ukiachilia kufuata utaratibu wa lishe iliyokamilika
wataalamu wanasema kinachofuata ni mazoezi ili kuuweka fiti na kuupa
nguvu ya kupambana na kila kinachokujambele yake.
Kwa maana hiyo, pamoja na kula mlo kamili, kunywa maji kwa wingi, bado
mwili unahitaji mazoezi ili kukamilisha kinga na uimara wa kujikinga na
marathi ya kuwa mwenye afya njema muda wote.
Kama ilivyo ni muhimu kuyafanya kuna vyakula pia ambavyo ni hatari kula
saa mbili baada ya kufanya mazoezi hasa vile vyenye sukari nyingi hatari
yake ni kuharibu kile chote ulichochokipata kwa kufanya mazoezi.
Wataalamu wa afya wamebainisha kuwa kutumia vitu vya sukari saa mbili
baada ya kufanya mazoezi huharibu mfumo mzima wa ulichokifanya kwa
makusudi ya kujenga mwili na badala yake huzalisha homoni bila mpangilio
wowote.
wameeleza kuwa utumiaji wa vyakula vya sukari hata hii ya majumbani saa
mbili baada ya kufanya mazoezi huvuruga mfumo wa homoni na ukuaji wa
mwili, huku ukiharibu mfumo wa urekebishwaji kwa kiwango cha sukari
mwilini unaoweza kukusababishia ugonjwa wa kisukari.
Pia wataalamu hao wamebainisha kuwa ni vyema baada kumaliza mazoezi kula
vyakula vyenye kiwango kidogo cha wanga ambavyo huepusha magonjwa ya
kisukari na magonjwa ya moyo.
Kwa hapa nyumbani, hivi vyakula vya wanga ni viazi, mkate mweupe, na hata muhogo.
Wataalamu hao wamesema kuwa mbali na vyakula vyenye sukari, ni vyema pia
kujiepusha kunywa juisi au vinywaji vingine baridi vyenye sukari ya
viwandani kwa sababu kujiepusha navyo ni kuepuka kubadili mpangilio
mzima wa mwili.
Ushauri huu ni mzuri kuzingatiwa hasa wale ambao wanafanya mazoezi kwa
lengo la kupunguza mwili kwani utakuwa wamefanikiwa kupunguza mafuta
huku ukiwa katika mpangilio mzuri pia hata wanaofanya mazoezi ya
kurekebisha mwili.
Muhimu kwa kila anayefanya mazoezi mara baada ya kumaliza ni kunywa maji mengi ili kurudisha yale yaliyotoka kwa njia ya jasho.
Sasa mara baada ya kufanya mazoezi tafadhali usitumie vitu hivi
– Maji ya baridi
– Chai
– Kula wali
– Soda
– Juisi
Ila baada ya mazoezi
– Kunywa maji ya kawaida
– Tulia kwa muda kabla ya kwenda kuoga
0 comments:
Post a Comment