WAKAZI
wa Mtaa wa Sechelela Kata ya Tambukareli Chadulu (A) Dodoma wanaotumia
dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV), wametakiwa kuepuka
matumizi ya unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na ngono uzembe.
Rai
hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sechelela,
Robarnt Pangaselo, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo.
Alisema
utumiaji wa dawa hizo na unywaji wa pombe, ngono zembe pamoja na
uvutaji wa sigara unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za dawa
hivyo kuwataka wakazi wa eneo hilo wanaojihusisha na unywaji wa pombe
hasa kwa wale wanaotumia dawa hizo kujiepusha.
“Changamoto
tunayokubaliana nayo ni matumizi sahihi ya dawa za ARV kwani kuna wale
ambao wamekuwa wakitumia dawa huku wakiwa wanakunywa pombe, wanavuta
sigara pamoja na ngono zembe, niwaombe wakazi kuachana na jambo hili,
tuendelee kuzitumia kwa kufuata masharti,” alisema
Hata
hivyo akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti huyo alisema kuwa
katika mtaa huo wanakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo ya
shule ya Medeli kutokana na uchakavu uliopo hali inayosababisha
hatari kwa watoto na walimu kuangukiwa na majengo ya shule hiyo.
Pangaselo
alisema kwa sasa hali ya uchumi katika Kata hiyo sio nzuri kutokana na
kuwa na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana hali ambayo imekuwa
ikirudisha maendeleo nyuma.
0 comments:
Post a Comment