Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye
filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo
huyo kwa uamuzi wake huo.
Akizungumza na mtandao huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule
ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti
maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza
ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM
mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu
barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza
kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama
hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki
kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka
2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha
ya Wema ni Ndumbagwe Misayo "Thea" (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara
Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).
0 comments:
Post a Comment