Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wakiwemo wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma, wamejikuta katika hali ya sintofahamu huku wengine wakimwaga machozi baada ya mbunge wa jimbo hilo, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo hilo.
Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 alikutana na wanachama wa chama cha mapinduzi Katika uwanja wa majimaji mjini Songea pamoja
na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo
hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini
pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika
jimbo la songea mjini.
Tamko
hilo la dkt. Nchimbi lilizua simanzi kwa baadhi ya wananchi na
wanachama wa CCM Songea huku wengine wakishindwa kujizuia na kujikuta
wakimwaga machozi.
Katika
maelezo yao wanachama hawa walisema kuachia ngazi kwa Dkt, Nchimbi
kutogombea katika jimbo hilo kunatoa fursa kubwa kwa vyama vya upinzani
kuchukua jimbo hilo hali ambayo hawakubaliani nayo.
Hata
hivyo wanachama hao walimuomba mbunge huyo kutengua msimamo wake na
kumtaka arejee tena kugombea jimbo la Songea mjini, jibu la dkt. Nchimbi
likawa anaenda kufikiria.
0 comments:
Post a Comment