Shirika la viwango Tanzania (TBS) lilianzisha huduma ya kukagua magari yaliyotumika kutoka nje ya nchi tangu mwaka wa 2002.
Lengo ni kuhakikisha magari yaliyotumika yanayoagizwa kutoka nje ya
nchi yanakidhi kiwango cha magari yaliyotumika na yanafaa kuendeshwa
barabarani. TBS imekuwa ikipata mawakala wa ukaguzi wa magari nje ya
nchi kwa kutangaza zabuni za kimataifa.
Kupima ubora wa bidhaa yakiwemo magari kwenye nchi zinakotengenezwa
au kutoka kabla ya kusafirishwa kuingia nchini husaidia kujua bidhaa
hizo yakiwemo magari kama yamekidhi kiwango, na kuwa hazina siyo hatari
kwa afya ya watumiaji na mazingira.
Huduma hii hurahishisha uingizwaji wa bidhaa na kuvikinga viwanda vya
ndani dhidi ya ushindani usio halali kutokana na uingizwaji wa bidhaa
hafifu.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuufahamisha umma wa
Watanzania na waagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya nchi kuwa
TBS wamesaini hati ya makubaliano na Taasisi ya Usafirishaji ya Taifa
(NIT), kwa ajili ya upimaji wa magari yote ambayo hayakukaguliwa ubora
wake katika nchi yalipotoka kabla ya kuingia nchini Tanzania.
Hivyo kuanzia tarehe 01-07-2015, NIT wataanza rasmi kupima magari yote yaliyoingia nchini bila kukaguliwa.
Gharama za ukaguzi na upimaji ni kama ifuatavyo;
1. Magari yanayotoka nchi ambazo TBS ina wakala wa upimaji wa magari yaliyotumika
N.B: Kiwango cha chini cha faini kitakachotozwa ni
TZS 800,000 Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuwakumbusha
waagizaji wa magari kutoka nchi za Uingereza, Japan na Umoja wa Falme za
Kiarabu kuwa ni lazima kukagua magari yote yaliyotumika kabla ya
kusafirishwa kuja Tanzania.
2. Magari yanayotoka nchi ambazo TBS haina wakala wa upimaji wa magari yaliyotumika
Waagizaji
wa magari yaliyotumika kutoka nchi ambako TBS haijateua wakala wa
ukaguzi hawatalipa faini bali watalipa ada ya ukaguzi USD 140 pamoja na
TZS 30,000 kama ada ya huduma.
Limetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P. 9524,
Dar Es Salaam,
Simu: +255(022) 2450206
Hotline:+0800110827
Barua pepe: info@tbs.go.tz
Tovuti: www.tbs.go.tz
0 comments:
Post a Comment