KITENDAWILI cha kumpata mgombea urais wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), huenda kikateguliwa kesho kwa vyama hivyo kumtangaza Dk. Wilbrod Slaa.
Ukawa inaundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na NLD.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya vikao vya Ukawa
vilivyofanyika mfululizo mwishoni mwa wiki, pamoja na mnyukano
uliokuwapo, hatimaye vyama hivyo vinatarajia kutoka na jina moja la
mgombea urais.
Akizungumza
na mtandao huu jijini hapa jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya
Ukawa, Benson Kigaila, alisema tangu awali Chadema walishakubaliana
kwamba mgombea wao ni Dk. Slaa.
“Ndani
ya Ukawa kinachofanyika ni maridhiano tu. Kwa Zanzibar tuliridhiana
tuwaachie CUF na wao waliridhia kuiachia Chadema Tanzania Bara. Kwa hiyo
kinachofanyika kwa sasa ni maridhiano ya ndani ya vyama,” alisema Kigaila.
Kuhusu
Dk. Slaa kutochukua fomu kuomba kugombea urais ndani ya chama kama
ilivyofanyika kwa viongozi wengine wa Ukawa, Kigaila alisema ni
utaratibu wa chama chenyewe.
“Tunapokutana kwenye vikao vya Ukawa si lazima waonekane wote wawe na fomu za kuomba urais, kila chama kina utaratibu wake,” alisema.
Wakati Ukawa wakijiandaa kuliweka hadharani jina la Dk. Slaa hapo kesho, huenda jiji la Dar es Salaam likawa na chereko katika kila kona kwani kesho hiyo hiyo Chama Cha Mapinduzi kimepanga kumtambulisha mgombea wao, Dk. John Magufuli kwa wananchi wa Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotangazwa mwishoni mwa Mkutano Mkuu wa CCM mjini
Dodoma jana mchana, baada ya Dk. Magufuli kutambulishwa kwa wakazi wa
Dodoma jana jioni, kesho itakuwa ni zamu ya wakazi wa Dar es Salaam.
Magufuli
ameteuliwa kuiwakilisha CCM katika kugombea urais baada ya kuwashinda
Dk. Asha Rose Migiro na Amina Salum Ali kwenye Mkutano Mkuu.
0 comments:
Post a Comment