Imeripotiwa
kutoka mkoani Simiyu katika Wilaya ya Bariadi kuwa Mkuu wa Wilaya (DC)
hiyo Bw. Ponsian Nyami amemuomba Rais Jakaya Kikwete asimwonee huruma na
badala yake atengue uteuzi wake kwa maana ameshindwa kusimamia ujenzi
wa maabara katika wilaya yake.
Aliyasema
hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Elaston Mbwilo katika kikao cha
majumuisho baada ya kutembelea maabara hizo na kubaini utekelezaji wake
ni asilimia 10 tu.
Kabla
ya kauli ya Nyami, Mbwilo alitoa lawama kwa DC kwa kushindwa kusimamia
ipasavyo agizo la Rais na kueleza kuwa ndani ya Mkoa, Wilaya hiyo ndiyo
ya mwisho katika utekelezaji wa agizo husika.
Hata
hivyo Mkuu huyo mkoa alisema kuwa viongozi pamoja na watendaji
wameshindwa kutekeleza agizo hilo ikiwa pamoja na miundombinu hasa
barabara ndani ya wilaya hiyo kuwa chini ya kiwango, ambapo alimtaka
Mkuu wa wilaya kuwachukulia hatua watumishi wote walisababisha hali
hiyo.
Hata
hivyo, Katibu Tawala wa Mkoa naye aliutupia lawama uongozi wa Wilaya
hiyo kwa kushindwa uwajibka, huku akieleza kuwa maabara zilizojengwa
ziko chini ya kiwango.
Baada ya viongonzi hao kuongea, Mkuu wa Wilaya, Nyami alisema:
“Namuunga
mkono Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa. Ni kweli tumefanya vibaya,
makosa haya ni makosa yangu mimi na wala sina haja ya kuomba msamaha.
Niko tayari kuwajibishwa kwa lolote lile na kwa wakati wowote maana
nilipoteuliwa nilihaidi kuwa nitaisimamia na kuiheshimu, sasa naona
nimeshindwa na usinionee huruma. Nakiri nimeshindwa.”
Nyami
alibainisha kuwa yeye kama kiongozi Mkuu ndani ya wilaya hiyo haoni
haja ya kuonewa huruma, kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi huo ikiwa
pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi wake.
0 comments:
Post a Comment