WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalum Prof.Mark Mwandosya amesema sio kitendo kizuri kwa wabunge wa upinzani kususia Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete atakapokwenda kuvunja Bunge hilo leo.
Akizungumza
bungeni mjini Dodoma jana wakati akichangia Mswada wa Sheria wa
Kuanzisha Tume ya Utumishi wa Walimu alisema si jambo zuri hata kidogo
kwa jambo kubwa la Taifa kama hilo kufanyika bungeni lakini wabunge wa
upinzani kutokuwepo.
Alisema
tangu kuwepo kwa wapinzani katika Bunge hilo kumeimarisha demokrasia
lakini kupingana kwa hoja ndio jambo la msingi lakini ni muhimu pia
mawaziri wakahudhuria vikao vya Bunge.
Prof.Mwandosya
alisema hili litakuwa Bunge lake la mwisho la kuwatumikia wananchi hasa
wa Jimbo la Rungwe Mashariki kwa vipindi vitatu mfululizo na
kuchaguliwa bila kupingwa
"Ujio
wa Rais ndani Bunge ni jambo zito na muhimu sana hasa kwa Taifa lakini
haiwezekani Rais anakuja kuvunja Bunge wapinzani hawapo si jambo zuri
lakini sio kila kitu kinacholetwa na Serikali lazima wapinzani wapinge
wakati mwingine ni kushindana kwa hoja tu," alisema Prof.Mwandosya.
Alisema
Demokrasia sio kupingana kila kitu lakini pia kwa Mswada huo wa
kuanzisha Tume ya Walimu ni wazi kuwa Serikali inajali sana walimu kwani
mishahara ya walimu italipwa na Serikali.
"Namshukuru
sana Rais Kikwete na viongozi wengine kwa kunichagua mimi kuwa Waziri
katika awamu tatu lakini pia nawashukuru wabunge wote kwa muda wote
niliokaa hapa bungeni kwani sitakuwepo tena katika bunge lijalo na
nimekuwa mbunge kwa miaka 15 sasa,"alisema Pfro.Mwandosya.
0 comments:
Post a Comment