WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya RaisKamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo inakutana kuchuja majina ya makada wake 38 waliorejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho na majina 33 ni lazima yapigwe panga ili kupeleka majina matano kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupigiwa kura.
Kwa
mujibu wa habari kutoka mitandao ya kijamii, kwenye vijiwe na mijadala
sehemu mbalimbali, majina hayo matano yanaaminika kwamba yatatoka
miongoni mwa watiania 10 ambao wametajwa zaidi katika mijadala hiyo.
Sababu
kuu mbili ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye mijadala hiyo na hata na
baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa Tanzania ni mbili. Mosi, uzoefu
wao ndani ya ungozi wa serikali na pili, nafasi yao ndani ya chama, ama
kama wajumbe wa NEC au Kamati Kuu.
Majina
ambayo yanatazamiwa kwamba yanaweza kupenya Kamati Kuu ni pamoja na
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal; Waziri Mkuu wa zamani na
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Stephen Wasira; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose
Migiro; Waziri Mkuu Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi
Maalum), Profesa Mark Mwandosya; Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani;
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Ujenzi, John
Magufuli;.
Kwa
ujumla kundi la makada hao (hapo juu) kila mmoja ana nafasi ya kupenya
kwenye mchujo wa Kamati Kuu, lakini pia anakabiliwa na changamoto
kadhaa.
Bilal
Dk.
Bilal ni Makamu wa Rais, katika hali ya kawaida ni vigumu msaidizi
namba moja wa rais aliyeko madarakani kukosa nafasi ya kupenya ngazi
hiyo hata kama ni kwa sababu tu za kiprotokali .
Mbali
na wadhifa wake, Bilal anayetoka Zanzibar amepata kuwa Waziri Kiongozi
na ana uzoefu wa kuendesha serikali, kwa maana hiyo anawakilisha kundi
la upande mmoja wa Muungano na hivyo siyo rahisi jina lake
kutokuzingatiwa.
Hata hivyo, Bilal ana changamoto ya umri kwani kwa umri wa miaka 70 alio nao sasa inakuwa ni kazi kubwa kukimbizana na changamoto za sasa katika nafasi hiyo.
Hata hivyo, Bilal ana changamoto ya umri kwani kwa umri wa miaka 70 alio nao sasa inakuwa ni kazi kubwa kukimbizana na changamoto za sasa katika nafasi hiyo.
Lowassa
Lowassa
ni mbunge wa Monduli, lakini pia alipata kuwa Waziri Mkuu hadi
alipojiuzulu Februari 2008 kutokana na kadhia ya Richmond juu ya mkataba
wa kufua umeme.
Hata hivyo, kadri muda ulivyosonga hadi sasa kadhia hiyo ilikuja kujidhihirisha kusukumwa zaidi na misuguano ya ndani ya CCM hasa juu ya chuki za nafasi ya uwaziri mkuu.
Hata hivyo, kadri muda ulivyosonga hadi sasa kadhia hiyo ilikuja kujidhihirisha kusukumwa zaidi na misuguano ya ndani ya CCM hasa juu ya chuki za nafasi ya uwaziri mkuu.
Kama
walivyo watia nia wengi, ni mjumbe wa NEC, amekuwa waziri katika
serikali ya Mzee Ali Hassan Mwinyi na ya Rais Benjamin Mkapa, anaijua
serikali vizuri.
Lowassa
amekuwa gumzo kubwa miongoni mwa watia nia wote kiasi cha kuandamwa
hata na wapinzani wake ndani ya chama kwa kuwa tu kila wakati kura za
maoni zimeonyesha kuwa ni chaguo la kwanza la wananchi katika kundi la
wawania urais wote, ndani ya CCM na hata ndani ya upinzani.
Mwanasiasa
huyo ambaye wengi waliamini kwamba kadhia ya Richmond ilikuwa
imemmaliza, aliigeuza hali hiyo kiasi cha kuonekana kuwa mtu
anayestahili kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mvuto wake kwa wananchi wengi, umefanya wapinzani wake wajipange kumwandamana kwa tuhuma mbalimbali, ambazo amezipuuza.
Mvuto wake kwa wananchi wengi, umefanya wapinzani wake wajipange kumwandamana kwa tuhuma mbalimbali, ambazo amezipuuza.
Wakati
wa mchakato wa kutafuta wadhamini ndani ya CCM, Lowassa alionyesha kwa
vitendo halisi jinsi anavyoungwa mkono na wanaCCM wenzake, kwani
mikutano yake iligeuka kuwa ‘mafuriko’ kila mkoa alikokwenda.
Alidhaminiwa na wanachama zaidi ya laki nane.
Lowassa
anaungwa mkono na wananchi wengi kwa sababu ni miongoni mwa viongozi wa
serikali wachache ambao wanatenda kwa vitendo halisi kuliko kupiga
kelele kwenye majukwaa ya kisiasa.
Anakumbukwa
kwa ufuatiliaji wa karibu kwenye kila wizara aliyokuwa, anakumbukwa kwa
kusaidia Tanzania kunufaika na maji ya ziwa Victoria na wakati akiwa
Waziri Mkuu alianza kubadili mfumo wa utendaji serikalini kutoka
‘business as usual’ na kuibua ari ya kufanya kazi kwa bidii zaidi
miongoni mwa watumishi wa umma.
Wassira
Wasira
ni miongoni mwa makada wa siku nyingi wa CCM, amehudumu kama waziri
katika serikali za awamu tatu, ya Mwalimu Nyerere; ya Mzee Mwinyi na ya
awamu ya nne, inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
Ni
miongoni mwa wanasiasa wakongwe, akiwa amejizolea umaarufu ndani ya CCM
na hata kwenye upinzani kwani mwaka 1995 alihamia NCCR-Mageuzi na
kugombea ubunge jimbo la Bunda na kumshinda, Jaji Joseph Warioba.
Hata hivyo, baadaye mahakama kuu ilitengua ubunge wake na kumtia hatiani kwa kuhusika na vitendo vya rushwa katika uchaguzi.
Hata hivyo, baadaye mahakama kuu ilitengua ubunge wake na kumtia hatiani kwa kuhusika na vitendo vya rushwa katika uchaguzi.
Ingawa
kiutendaji Wasira anaonekana kama mmoja wa watu wanaojituma, kitendo
chake cha kuhama CCM na kurejea tena kinaweza kuwa moja ya sababu za
kutumika dhidi yake.
Membe
Amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje tangu mwaka 2007 alipoondoka Dk. Migiro kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).
Membe aliingia bungeni mara ya kwanza mwaka 2000 wakati wa utawala wa Mkapa, lakini ni chini ya Kikwete alipata nafasi ya kuwa Naibu Waziri, akianzia Mambo ya Ndani na baadaye Nishati na Madini kabla ya kuibukia Mambo ya Nje kama waziri kamili.
Membe aliingia bungeni mara ya kwanza mwaka 2000 wakati wa utawala wa Mkapa, lakini ni chini ya Kikwete alipata nafasi ya kuwa Naibu Waziri, akianzia Mambo ya Ndani na baadaye Nishati na Madini kabla ya kuibukia Mambo ya Nje kama waziri kamili.
Ni
mjumbe wa NEC kama walivyo makada wenzake. Kwa miaka mingi ya utumishi
wake Membe ambaye pia ni ofisa wa usalama wa taifa, alifanya kazi nje ya
nchi.
Duru
za kisiasa nchini zinasema kuwa ingawa hana mizizi mirefu ndani ya
chama, kukaa kwake wizara ya Mambo ya Nje kwa muda huo kumempa uzoefu wa
uendeshaji wa serikali.
Hata hivyo kumekuwa na maoni kuwa Membe anabebwa na wakuu serikalini.
Hata hivyo kumekuwa na maoni kuwa Membe anabebwa na wakuu serikalini.
Migiro
Huyu
ni mwanamke pekee anayepewa nafasi ya kufika mbali miongoni mwa watia
nia wote kwa sababu ya nafasi yake, kwanza ndani ya nchi na nje
alipokuwa UN. Anaelezwa kuwa na uzoefu wa ndani na wa kimataifa.
Katika
kipindi hiki ambacho Rais Kikwete amekuwa anatoa fursa nyingi zaidi kwa
wanawake katika vyombo vya maamuzi, Dk. Migiro anaweza kupenya kwenye
kundi la tano bora hivyo kusaka kura za NEC kama anataka kufika kwenye
tatu bora kwenye mkutano mkuu.
Pinda
Huyu
ni waziri mkuu tanu Februari 2008 alipojiuzulu Lowassa. Pinda amekuwa
mbunge tangu awamu ya pili ya Rais Mkapa na kuwa waziri wa Tamisemi.
Muda
wake mwingi wa utumishi alikuwa ndani ya Ikulu kama ofisa wa serikali.
Ni mwanasiasa ambaye kimsingi hajawa na kishindo sana licha ya nafasi
yake kubwa ya uwaziri mkuu.
Pinda
amekuwa miongoni mwa mawaziri wakuu wapole ambao hawajaacha kishindo
kama alivyokuwa Waziri Mkuu pekee wa Rais Mkapa, Sumaye ambaye alikaa
kwenye nafasi hiyo kwa miaka 10, lakini hakuacha kishindo chochote pia.
Hata
hivyo, kwa sababu za itifaki kama ilivyokwa Dk. Bilal, itakuwa ni
vigumu kumpiga panga jina lake katika ngazi ya Kamati Kuu, ingawa wote
umri nao umesogea, Bilal miaka 70 na Pinda miaka 67.
Mwandosya
Mwandosya
ni mwanasiasa aliyeweka rekodi mwaka 2005 kwa kuingia tatu bora katika
kinyang’anyiro cha urais, akiachwa nyuma na Kikwete na Dk. Salim Ahmed
Salim.
Amekuwa
moja ya nguzo ya siasa ya CCM kwa miaka mingi na ndiye alianzisha
mkakati wa harambee ya kuchangia chama kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2005.
Amehudumu
katika awamu mbili kama waziri, awamu ya tatu na ya nne. Kwa kitambo
alikuwa ndiye nguzo ya wanaCCM mkoani Mbeya, lakini kuibuka kwa Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, kama mmoja
wa watia nia, kumeibua maswali mengi kama Profesa Mwandosya bado
anashikilia nafasi hiyo Mbeya na kanda yote ya nyanda za juu kusini.
Hata hivyo, umri wa miaka 66 wa Mwandosya siyo haba katika dunia ya leo inayohitaji mchakamchaka.
Hata hivyo, umri wa miaka 66 wa Mwandosya siyo haba katika dunia ya leo inayohitaji mchakamchaka.
Sumaye
Sumaye
aliweka rekodi ya waziri mkuu aliyekalia kiti hicho mfululizo kwa muda
mrefu zaidi ya mawaziri wakuu tisa kuwahi kuteuliwa tangu uhuru.
Hakuna
ubishi kwamba Sumaye ana uzoefu wa kuendesha serikali, amekuwa naibu
waziri, waziri na waziri mkuu kwa miaka 10. Alishikilia ubunge wa jimbo
la Hanang hadi alipoamua kustaafu mwaka 2005 baada ya kuliwakilisha kwa
miaka 20.
Ingawa
Sumaye hana kikwazo chochote cha kisiasa kupenya hatua ya Kamati Kuu,
nguvu zake za kisiasa jimboni kwake zimepungua ndiyo maana mwaka 2012
alibwagwa katika nafasi ya UNEC na Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais (Mahisiano na Uratibu).
Magufuli
Dk. Magufuli amekuwa ni miongoni mwa mawaziri wachache wachapakazi tangu awamu ya Rais Mkapa na hata sasa.
Amekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na kisha Waziri wa Ujenzi wakati wa Mkapa na chini ya Kikwete amekuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo, kisha wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kila alikopelekwa amejitahidi kuchapa kazi.
Amekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na kisha Waziri wa Ujenzi wakati wa Mkapa na chini ya Kikwete amekuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo, kisha wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kila alikopelekwa amejitahidi kuchapa kazi.
Ni
kati ya mawaziri wanaozijua wizara na majukumu yao sawasawa, ni
mfuatiliaji. Kwa utendaji huo, Magufuli amejijengea sifa ya kuwajibika
kama kiongozi.
Hata hivyo, kuna jambo kubwa ambalo limekuwa likiibuka kila wakati juu ya kuhusika kwake na uuzaji wa nyumba za serikali.
Ingawa inadaiwa kuwa ulikuwa uamuzi wa baraza la mawaziri, bado wananchi wengi wamekuwa wakihoji uamuzi wa kuuza nyumba hizo.
Ingawa inadaiwa kuwa ulikuwa uamuzi wa baraza la mawaziri, bado wananchi wengi wamekuwa wakihoji uamuzi wa kuuza nyumba hizo.
Mbali ya kuwa mbunge wa Chato tangu mwaka 1995, Magufuli hajawahi kugombea nafasi nyingine ya kuchaguliwa ndani ya CCM.
Siyo mjumbe wa NEC na hakuna kumbukumbu zozote kwamba alipata kuomba nafasi hiyo.
Siyo mjumbe wa NEC na hakuna kumbukumbu zozote kwamba alipata kuomba nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment