MSTAHIKI
Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amesema hana sababu ya
kuendelea kujibizana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
(Chadema), kwani amekuwa akimpa changamoto za kiutendaji ambazo
zimemfanya kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema,
mbunge huyo anaapswa kusubiri kubali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), ili aweze kutumia vema jukwaa la kisiasa kuliko ilivyo sasa
anavyotumia Bunge kuwachafua watu wengine.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Mbeya, Meya Kapunga, alitumia nafasi
hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu hali halisi ya utendaji kazi wake uliokuwa
umezungukwa na majungu, chuki na fitina zisizokuwa na msingi
zinazoendelea kutolewa na Mbunge ‘Sugu’ ambaye alimfananisha sawa na
chipukizi wa kisiasa.
“Leo
(jana), asubuhi nimemsikia Sugu, akizungumza bungeni kuhusu ugawaji wa
Jimbo la Mbeya Mjini na kunitaja mimi ni miongoni mwa viongozi
wanaoshinikiza kugawanywa kwa jimbo hili, wala sikatai ni kweli kwani
mchakato huu wa kuligawa jimbo hili niwa muda mrefu kabla ya Sugu
kuingia ulingoni,” alisema Kapunga
Alisema,
mchakato wa kuligawa jimbo hilo, ulianza mwaka 2008 ukiwa chini ya
Mbunge Mpesya hivyo yeye kama Meya ni jukumu lake kulisemea hilo kama
mtendaji wa halmashauri.
“Hapa
kosa langu nini mpaka Sugu kunisema bungeni, kwanza nimeona ni mtoto
anayezoea tabia mbaya, kukaa kila saa ananisema bungeni anaonyesha ni
jinsi gani asivyokomaa kisiasa,” alisema
Alisema,
Sugu ni mjumbe wa vikao vya kiutendaji vya halmashauri ana nafasi kubwa
ya kufika na kuyazungumzia hayo tatizo linalomsumbua ni upeo wake mdogo
wa kufikiri hivyo kujiaminisha kwambajimbo la Mbeya ni mali yake.
Alisema,
Mbeya ni mali ya wananchi, si la ukoo na kitendo cha kuwaza jimbo ni
mali yake ni ujinga, yeye atabaki kuwa kwenye orodha ya wabunge wa
ajaabu ambao kila siku kazi yake ni kumuwaza Kapunga badala ya kusimama
na hoja.
“Mimi
ninamsubili huku kwa wananchi, sasa ngoja nimuache tu aendelee na utoto
na jambo la kumsikitikia ni kwamba mpaka leo anaamini akili za wanambea
wa miaka mitano iliyopita ziko palepale,” alisema
0 comments:
Post a Comment