Mtangazaji mahiri wa
Kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa ya
TBC1, Mboni Masimba, amejikuta akiangua kilio kwenye Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar, alipotembelea wodi ya wazazi na kusimulia
jinsi ambavyo daktari alimweleza kuwa ilikuwa kiduchu tu afe wakati wa
kujifungua hivi karibuni.
Mtangazaji mahiri wa Kipindi cha The Mboni Show, Mboni Masimba akihojiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akiwa wodini hapo
juzikati, Mboni ambaye pamoja na timu yake walikwenda kwa ajili ya
kukabidhi vifaa mbalimbali vya msaada kwa akina mama ambao wapo kwenye
wodi hiyo, alisema kuwa hospitali ambayo ni ya uhakika ni Muhimbili
pekee kwani ndiyo walionusuru uhai wake.
“Daktari alinieleza
kuwa mimi nilikuwa ni wa kufa jamani hapa ndipo niliporejeshewa uhai
wangu tena japokuwa nilijifungulia hospitali nyingine lakini huko kote
walishindwa, hapa ndipo walinitibu pekee na niliweka ahadi kuwa nitarudi
kwa ajili ya kutoa kwa wengine,” alisema Mboni.
Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Uzazi, Dk. Mathew Kalianga alisema kuwa ugonjwa uliompata
Mboni kitaalam unaitwa Pulmonary Embolism ambapo mara nyingi watu
wanaopata ugonjwa huo ni asilimia tano tu kati ya mia ndiyo wanapona
hivyo Mboni ni mmoja aliyebahatika.
Pulmonary Embolism ni
ugonjwa wa Kuganda kwa damu ambao husababisha mshipa mkubwa
unaosafirisha damu na hewa kwenda kwenye mapafu kuziba. Hali hiyo huweza
kusababisha mtu kufariki dunia ghafla. Ndiyo uliomuua mwanamuziki wa
Nigeria marehemu Goldie.
Mboni aliyesindikizwa
na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alitoa msaada wa mashuka,
viti vya matairi na vingine vingi vinavyohitajika wodini hapo.
0 comments:
Post a Comment