Kumekuwa na msururu wa mashambulizi ya maguruneti kuwalenga maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.
Maguruneti
hayo yalirushwa katika maeneo ambayo yaliathiriwa na maandamano ya
ghasia kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa
tatu.
Maafisa wa polisi wamewalaumu wanaharakati wa upinzani.
Makundi
ya haki za kibinaadamu yanasema takriban watu sabini wameuawa na
wengine 500 kujeruhiwa tangu maandamano hayo yaanze mnamo mwezi Aprili.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment