Pages

Ads 468x60px

Saturday, June 20, 2015

Wema Sepetu awa kivutio mkutano wa CCM nyumbani kwao Ikungi


Malkia wa urembo nchini Tanzania kwa mwaka 2006, ambaye pia ni msanii maarufu wa sinema hapa nchini, Wema Sepetu, amegeuka gumzo mkoani Singida, baada ya kutinga kijijini kwao Ikungi, kwa ajili ya kutimiza haki yake ya kikatiba ya kujiandikisha kwa ajili ya kuweza kushiriki kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Wema, ambaye alikuwa ameongozana na mama yake mzazi, na ambaye ameeleza kuwa ameamua kujiandikisha huko kwakuwa ndio asili yake, alikuwa kivutio katika kituo alichojiandikishia, kabla ya kushiriki pia kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM, katika kata ya Ikungi, mkoani Singida.
Hapa ni picha za matukio mbalimbali wakati wa shughuli hiyo, kama zilivyonaswa na kamera ya Jukwaa Huru
SAM_0073Ni Miss Tanzania 2006 na msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu mara baada ya kufika kwenye kituo cha kujiandikisha kilichopo katika shule ya sekondari Ikungi.
SAM_0075Ni Mama mzazi wa Wema Sepetu,Bi Mariamu Sepetu (wa kwanza kutoka kushoto waliosimama) wakishauriana jambo na binti yake wakati wakisubiri maelekezo ya utaratibu wa kujiandikisha.
SAM_0082Ni Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu(wa kwanza kutoka kulia) akiwa na mama yake mzazi wakishauriana kwenda kituo kingine baada ya kuona kituo cha kwanza walichojipanga kilikuwa na idadi kubwa ya watu.
SAM_0083Ni Mama mzazi wa Wema Sepetu(yupo nyuma ya mwanaume aliyevaa suti nyeusi mbele yao) wakiongozana na motto wake kwenda kwenye kituo kingine cha kujiandikisha ili waweze kuangalia iwapo idadi ya watu haitakuwa kubwa.
SAM_0077Ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu kwenye vituo vilivyotengwa katika shule ya sekondari Ikungi wakisubiri kujiandikisha
SAM_0085Ni Mama mzazi wa msanii wa Bongo Movie(wa kwanza kutoka kushoto aliyekaa)akisubiri zamu yake ya kujiandikisha baada ya kufanikiwa kuingia kwenye chumba cha kujiandikisha.
SAM_0094Ni Miss Tanzania 2006 na msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu (wa kwanza kutoka kulia akiendelea kuchati na marafiki zake wakati akisubiri zamu yake ya kujiandikisha.
SAM_0099Ni Miss Tanzania 2006 na msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu( wa pili kutoka kushoto kwa karani anayeandikisha)akisubiri kusaini kwenye fomu maalumu huku mama yake mzazi akimwangalia wakati wa zoezi hilo likiendelea.
SAM_0102Ni Bi Wema Sepetu akisaini fomu baada ya kukamilisha taratibu ya kujiandikisha.
SAM_0108Ni Mama Sepetu(wa kwanza kutoka kushoto aliyekaa) akiwa na Miss Tanzania 2006,Bi Wema Sepetu wakisubiri kwenda kwenye mashine ya BVR kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiandikisha.
SAM_0112Ni Mbunge wa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA)Bwana Tundu Lissu(wa kwanza kutoka kushoto) akizungumza na mama mzazi wa Miss Tanzania 2006 na msanii wa Bongo movie,mama Wema Sepetu (wa pili kutoka kulia) na wa tatu kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu,wakizungumza wakati wakisubiri kukamilisha taratibu za uandikishaji.Mbunge huyo alipitia kwenye kituo hicho alipokuwa katika zoezi la kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili waweze kuwa na uhalali wa kupiga kura wakati utakaapowadia.
SAM_0116Ni Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu akisani dole humba kwenye mashine ya BVR kukamilisha zoezi la kujiandikisha.
SAM_0121Ni Mama mzazi wa Wema Sepetu akisaini dole gumba kwenye mashine ya BVR kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye kituo cha shule ya sekondari Ikungi,Mkoani Singida.
SAM_0060
SAM_0065Ni Msanii wa Bongo Movie na Miss Tanzania 2006,Bi Wema Sepetu katika mapokezi yake alipofika kwenye viwanja vya ghala ulipofanyika mkutano wa hadhara
SAM_0052Ni Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu akipokea maelekezo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Bwana Alluu Ismaili Segamba kabla ya kuongea na wananhi pamoja na wanachama waliohudhuria kwenye mkutano huo.
SAM_0058Ni Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Wema Spetu (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kuimba wimba wa kimila mara baada ya kukaribishwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi kujiandikisha

0 comments:

Post a Comment

SHARE