Rais
wa Jamhuri ya Muungano, Dkt Magufuli ameagiza viongozi wa Wizara ya
Nishati na Madini, Manaibu wake, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Makatibu
Wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Maafisa wa TRA, na watumishi
wengine waliohusika katika upotevu wa matrilioni ya fedha kupitia sekta
ya madini wahojiwe.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu alipokuwa akipokea ripoti ya pili ya
kamati iliyokuwa ikichunguza makinikia yaliyopo kwenye makontena
bandarini iliyoundwa na wanasheria ya wachumi.
Akizungumza
kwa uchungu, Rais Magufuli alisema kuwa Tanzania imejaliwa na kila aina
ya madini ambayo unaweza kuyataja hadi ukasahau lakini bado sisi ni
maskini.
Akitaja
baadhi ya madini alisema kuna dhahabu, almasi, tanzanite, gesi za kila
aina na vitu vingine mbalimbali lakini tumebaki masikini kutokana na
viongozi kutokuwa wazalendo.
Akisoma
ripoti hiyo Ikulu leo, Mwenyekiti wa Kamati, Prof. Nehemiah Osoro
alisema kuwa Mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini wa kipindi
kilichopita walisaini mikataba ya madini ambayo haikuwa na faida kwa
taifa na hivyo kusababisha nchi kupoteza mapato kwa kutoa misamaha ya
tozo mbalimbali.
Prof.
Osoro alieleza zaidi kuwa kwa kutumia mamlaka aliyonayo, Mawaziri
waliopita wamekuwa wakiwaongezea muda wa kufanyakazi au eneo la
uchimbaji makampuni ya madini bila kufuata sheria. Akitolea mfano hapa,
Prof. Osoro alisema kuwa, Waziri Prof. Muhongo alifanya hivyo kwa mgodi wa North Mara.
Aliyekuwa
Waziri wa Nishati na Madini kipindi cha mwisho cha Rais Mkapa, Daniel
Yona amewahi kushtakiwa kwa kosa la kuongezea mkataba wa ukaguzi wa
madini kampuni MS ALEX STUWART kwa miaka miwili zaidi kuanzia
tarehe 14 Juni 2005 hadi tarehe 23 Juni 2007 bila kufuata utaratibu.
Rais
ameagiza viongozi hao wahojiwe ili waeleze kwanini walifanya
waliyoyafanya na kwa manufaa ya nani kitu kilichopelekea taifa kupoteza
fedha nyingi.
Miongoni mwa watakaohojiwa kufuatua amri hii ya Rais ni, William Ngeleja, Prof. Sospeter Muhongo, Nazir Karamagi, Daniel Yona, Andrew Chenge, Fredrick Werema, Johnson Mwanyika.
0 comments:
Post a Comment