Taarifa
ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo
kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Joseph
Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na
inafanya kazi kinyume cha sheria.
Prof.
Osoro amesema kwamba Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa
kufanya shughuli zake hapa nchini na imetenda makosa yakiwemo
kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara
taifa.
Aidha
Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi
hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku
ikiongeza kwamba katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali
haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.
Prof.
Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza
ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya
mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11,
bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini kwenye makontena
yote 44,277 tangu mwaka 1998 ni Tsh. tril 132.56.
Pamoja
na hayo imebainika kuwa uongezwaji wa leseni kinyume cha sheria ambapo
imedaiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na
Sospeter Muhongo ndio waliohusika na uongezaji wa muda kwenye uchimbaji
wa madini.
Kamati
hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kuchukua sheria juu ya
kampuni ya ACACIA iliyopo nchini kinyume cha sheria kupitia msajili wa
makampuni ikiwa ni pamoja na Mawaziri wote walioshiriki kwa namna moja
au nyingine juu ya mikataba ya uchimbaji madini huku ikiitaka Serikali
iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye makampuni ya madini
0 comments:
Post a Comment