Baada ya kuzushiwa kifo ,muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Banza Stone amesema si jambo la busara la kuzushiana kifo
Akizungumza kwenye AMPLIFAYA ya Clouds Fm jana june 24 alisema: "Mimi
nilikuwa nasumbuliwa na kichwa sana na ki homa homa fulani kama miezi
miwili lakini saaa hivi niko vizuri, naelendele poa na leo nilienda
hospitali daktari kufanya sound check akaniambia kuwa malaria"
Mtangazaji:…Jana ilikua ni mara ngapi kuzushiwa kifo ?
Banza Stone:.."Mimi
hata sijui ila nasikia mara watu oooh banza kafa, mara ooh kila mtu
anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima naweza kufanya kazi ila kwasasa
siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili mwangu"
Mtangazaji: Vipi kuhusu kazi zako za muziki bado unaendelea nazo ama au ??
Banza Stone:….."Naweza
kusema ninaendelea na muziki kama kawaida kwasababu sasa hivi nina kama
nyimbo sita mpya ziko ndani kesho, kesho kutwa naweza nikaamua niachie
moja mpaka video ziko tayari sio za bendi bali ni zangu binafsi…"
0 comments:
Post a Comment