ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba
amesema hatoongea chochote kinachohusu masuala ya uongozi katika kipindi
hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Oktoba.
Jaji
Warioba alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa
kampeni ya Vuguvugu la Uhuishaji Maadili inayofanywa na chama cha
wataalam Mbalimbali wa wakristo(CPT)alipotakiwa kutoa maoni kuhusu
mchakato wa uchukuaji fomu za kugombe urais unaoendelea katika Chama Cha
Mapinduzi(CCM).
Alisema
katika kipindi hiki cha mchakato wa kuelekea katika uchaguzi mkuu sio
raisi mtu akaongea jambo la msingi likaeleweka katika jamii.
“Nilisema
kwa kipindi hiki nitakaa kimya sitoongea,kwa sababu muda huu ukisema
chochote kinahusishwa na uchaguzi mkuu jambo ambalo sitaki
linitokee,hata hapa nimekubali mwaliko huu kwa sababu ya ushawishi ha
heshima ya rafiki yangu (Profesa Kanywanyi)”alisema Jaji Warioba.
Alisema
hakubaliani na baadhi ya watangaza nia wanaojiita waadilifu kwakuwa
kuna baadhi yao wanatoa rushwa na wengine wanafuata taratibu za kawaida
katika mchakato huo.
Alisema
kulingana na misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
kila mtanzania anapaswa kuwa mzalendo na mwajibikaji.
Alisema
mgongano wa maslahi katika baadhi ya maeneo ni chanzo cha ufisadi
kuporomoka kwa maadili mambo ambayo yanaweza kuhatarisha amani ya nchi.
“Viongozi na jamii kwa ujumla wanapaswa waichunge amani iliyopo nchini kwakuwa ikipotea itakuwa aibu kwa Taifa,”alisema Warioba.
Alisema
kwa sasa kuna dalili ya ukabila,udini na ubaguzi wa rangi,kikanda na
wakichama unaanza kurudi jambo ambalo linachangia kuhatarisha amani na
uporomoshaji wa maadili.
Alisema nchi haiwezi kuwa na viongozi wenye maadili endapo jamii inayowazunguka haina maadili.
“Jamii
haionyeshi kama inataka viongozi wenye maadili kwakuwa inachangia
kuporomosha maadili,hakuna mtu ambaye anaweza akamrekebisha mwenzake
katika hili,”alisema Jaji Warioba.
Awali
akitoa mada kuhusu suala la uhuishaji maadili Mwnyekiti wa CPT,Profesa
Beda Mutagahwya alisema kwa sasa Taifa limekuwa na kashfa mbalimbali
zinazohusisha watumishi wa umma na watawala ambao wengi wao
hawajachukuliwa hatua zozote za kinidhamu na kisheria.
“Kumekuwa
na wimbi la rushwa,uvunjaji wa haki za binadamu bila kuchukuliwa
hatua,uvunjaji wa haki za binadamu bila kuchukuliwa yote haya yanaamsha
hasira za umma na kutufanya tusema sasa yatosha,”alisema Profesa Mutagahwya.
Alisema
kitendo cha kutafsiri kama bahati mbaya ama ajali kazini kwa matukio
ya dhuluma na maovu ni kudalilisha Taifa kwakuonekana limekosa umakini.
Alisema kuna umuhimu wa kujenga upya maadili ya Taifa ambayo kwa sasa yameporomoka na kuhatarisha amani na maendeleo ya nchi.
Alisisitiza
wahusika wanapaswa kutunga miundo mipya ya utawala,sheria
mpya,kuimarisha vyombo vya usalama pamoja na kuunda tume za maadili na
taasisi za kuzuia rushwa.
0 comments:
Post a Comment