KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana ameendelea kusisitiza kuwa chama kinarudishwa kwenye misingi yake akitaka mtu anayefikiri misingi hiyo haifai, aondoke atafute mahala pengine.
Kinana ambaye katika ziara zake tangu akiwa Kagera, Geita na sasa
Mwanza, amekuwa akisisitiza viongozi wa CCM kuhudumia wananchi na
kuwatendea haki, alisema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara mjini
Sengerema.
“Nataka niwahakikishe watanzania tunakirudisha hiki chama kwenye
misingi. Na kama kuna mtu anafikiri misingi hiyo haifai, bora aondoke
kwenye CCM atafute mahala pengine pa kwenda,” alisema.
Akishangiliwa na umati wa watu uliohudhuria mkutano huo, Kinana
aliwataka wanasiasa kushikamana kusemea wanyonge. Alisema watu wengi
hawana vyama vya siasa isipokuwa wanalazimika kuingia kutafuta maisha.
Katibu Mkuu alisema wanachotaka ni kuhakikisha chama kinakuwa karibu na watu, kinawasikiliza na kuwasemea.
“Hiki ndicho chama tunachokijua sisi wengine,” alisema na kusihi wana
CCM kushikamana katika kusimamia misingi ya watu kwa kupinga mambo ya
hovyo na kuunga mkono mambo mazuri.
Alisema mtu anayekiri upungufu wake si mtu dhaifu bali ni imara. Alisema si kila jambo linapawa kukubaliwa.
“Watu wananyimwa haki yao, sawa, wanadhulumiwa, tuko mbioni,...nataka
niwahakikishie watanzania, tunakirudisha hiki chama kwenye misingi,”
alisisitiza.
Alisema kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira, watu wapate mahitaji yao. Pia alisema serikali inapaswa kusimamia sheria
0 comments:
Post a Comment