WAZIRI
Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina
lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama
chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa
Tanzania.
Lowassa
aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi
wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa
shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.
"Nimekuwa
mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya
kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza
kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata
jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa
jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi
tu". alisema Lowassa.
Lowassa
aliwasili Mkoani Ruvuma mapema jana mchana akitokea Mkoani Iringa
kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi
ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea
kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya
paa la jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza nao.
0 comments:
Post a Comment