IDARA
ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga imesema imebaini kuwabaadhi ya raia wa
kigeni wanatafuta mbinu ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura.
Imesema
imejipanga kuhakikisha raia hao hawapati nafasi yoyote ya kujiandikisha
huku ikiwaonya wakazi na waandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga
kura kupitia mfumo mpya wa BVR kuwa makini na wageni hao.
Ofisa
Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Anna- maria Yondani, aliwataka wakazi na
waandikishaji kufanya kazi kwa kushirikiana na kutoa taarifa pale
watakapobaini kuna raia anataka kujiandikisha.
Yondani
alisema uandikishaji ni mahsusi kwa raia wa Tanzania tu hivyo watu
wasio raia wa Tanzania wasithubutu kusogea eneo la uandikishaji kwa
kufanya hivyo hatua za sheria zitachukuliwa dhidi yao
0 comments:
Post a Comment