WAZIRI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe amesema kati ya mambo anayoweza kujivunia wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya nne ni kuwa miongoni mwa washauri wazuri wa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema ni mmoja wa mawaziri wanaomshauri katika kusimamia na
kutekeleza mambo ya maendeleo ambayo yamewezesha kuboresha huduma
mbalimbali za kijamii.
Aidha, amesema ni jambo la kusikitisha kuona kuna watu tena baadhi
yao wako ndani ya CCM wanajifanya hawajaona maendeleo ikiwemo kukamilika
kwa ujenzi wa barabara za lami zinazounganisha kati ya mkoa mmoja na
mwingine, maji, afya, elimu na mingineyo.
Alisema, serikali ya awamu ya nne inapaswa kupongezwa kutokana na
utendaji wake mzuri katika kubuni, kutekeleza na kufuatilia miradi yote
iliyopangwa na hiyo inampa sifa kubwa yeye na kumfanya kuwa miongoni mwa
watu wenye uwezo wa kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM.
Aliyasema hayo jana mjini Songea wakati akiwashukuru wanachama wa CCM
waliomdhamini katika harakati zake za kuomba ridhaa ya CCM ili awe
mgombea wake, huku akisisitiza kuwa anajiona ana sifa nyingi, ndiyo
maana amejitokeza aweze kuendeleza mema yaliyofanywa na Serikali ya Rais
Kikwete.
0 comments:
Post a Comment